IQNA

Wairani Milioni 3 Kushiriki Arubaini ya Imam Hussein AS Karbala, Iraq

13:12 - October 30, 2017
Habari ID: 3471238
TEHRAN (IQNA)-Wafanyaziara milioni tatu Wairani wanatazamiwa kufika katika mji mtakatifu wa Karbala, Iraq kwa ajili ya Arubaini ya Imam Hussein AS.

Akizungumza na waandishi habari Jumapili, mkuu wa ubalozi mdogo wa Iran mjini Karbala Mir Masoud Hosseinian amethibitisha kuwa idadi ya Wairani wanaoshiriki katika matembezi ya Arubaini mwaka hii ni takribani milioni tatu.

Aidha amesema Hilali Nyekundu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, IRCS, itawahudumia wafanyaziara katika matembezi hayo ya kila mwaka.

Arubaini ya mjukuu wa Mtume Muhammad SAW, Imam Hussein AS, ndio mjumuiko mkubwa zaidi ywa kidini duniani ambapo mwaka jana takribani wafanyaziara milioni 20 wa madhehebu ya Shia na Sunni walishiriki kutoka maeneo yote duniani.

Inafaa kukumbusha hapa kuwa, majlisi na ziara ya siku ya Arubaini hufanyika kila mwaka tarehe 20 Safar, kwa mujibu wa kalenda ya Hijria Qamaria, baada ya kupita siku Arubaini tangu tarehe 10 mwezi wa Muharram kwa ajili ya kukumbuka kuuawa shahidi mjukuu wa Mtume SAW, Imam Hussein AS na masahaba zake ambao walijitolea roho zao kwa ajili ya kuhuisha dini ya Mwenyezi Mungu katika jangwa la Karbala. Haram Takatifu ya Imam Hussein AS iko katika mji huo wa Karbala.

3657919/

captcha