IQNA

14:21 - December 12, 2017
News ID: 3471306
TEHRAN (IQNA)-Waislamu wamehimizwa kujifunza kuhusu mfumo wa Uchumi wa Kiislamu sambamba na mifumo mingine ya kiuchumi.

Wito huo umetolewa na Rais wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kiislamu cha Islamabad (IIUI) Dkt. Ahmed Yousaf al-Draiweesh.

Ameyasema hayo Jumatatu katika chuo hicho wakati akihutubu katika warsha ya siku mbili ya kimataifa kuhusi kuimarisha mfumo wa fedha wa Kiislamu.

Katika warsha hiyo, wataalamu wa masuala ya uchumi kutoka Brunei Darussalam, Saudi Arabia, Indonesia, Algeria, Malaysia, Ujerumani, Bosnia Herzegovina na nchi zingine. Washiriki walijadili kuhusu nafasi ya mfumo wa fedha wa Kiislamu katika ustawi wa kijamii-kiuchumi na kuwawezesha wanawake kiuchumi.

Dkt. Al-Draiweesh amesema umasikini duniani umesababishwa na kuwepo riba katikamfumo wa benki na kupuuza Zakat. Aidha amewahimiza vijana Waislamu kuzingatia suala la kusambazwa utajiri kwa uadilifu na kujizuia na riba.

Aidha alitoa wito kwa wataalamu wa masuala ya uchumi wa Kiislamu kubuni mbinu za mfumo endelevu wa kifedha na kuimarisha nafasi ya benki za Kiislamu.

3464670

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: