IQNA

Malta yaazimia kuimarisha mfumo wa Kiislamu wa kifedha

11:37 - June 29, 2018
Habari ID: 3471576
TEHRAN (IQNA)-Serikali ya Malta imeanzisha bodi ya kitaifa kwa lengo la kustawisha mfumo wa Kiislamu wa kifedha ambapo sheria mpya zitatungwa kuwavutia wawekezaji Waislamu nchini humo.

Malta, ambayo ni nchi ndogo zaidi katika Umoja wa Ulaya, inaweka mkakati wa kuwa kitovu na hebu ya mfumo wa Kiislamu.

Jumuiya ya Mfumo wa Kiislamu wa Fedha Malta imesema itashirkiana na bodi husika za kitaifa ili kufanikisha mkakati huo.

Silvio Schembri katibu wa kamati ya bunge ya huduma za kifedha, uchumi wa kidijitali na ubuni amesema: "Serikali ya Malta inapanga kuwasilisha marekebisho ya sheria ili kuruhusu taasisi ya Kiislamu za kifedha ziweze kuwa na mahusiano na nchi za Umoja wa Ulaya, kati ya fursa zinginezo."

Mfumo wa Kiislamu wa fedha unaharamisha riba na hivyo unaendelea kuwavutia watu wengi duniani. Inakadiriwa kuwa mfumo wa Kiislamu wa kifedha sasa una ukubwa wa dola trilioni mbili kote duniani kuanzia Asia Magharibi (Mashariki ya Kati), Afrika na Kusini mashariki mwa Asia.

3466183

captcha