IQNA

13:40 - December 25, 2017
News ID: 3471324
TEHRAN (IQNA)-Asilimia 12.5 ya watu katika kila mkoa nchini Iran wanatazamiwa kuhifadhi Qur'ani kikamilifu ifikapo mwaka 2025, kwa mujibu wa mkakati uliowekwa.

Katika taarifa Bw. Mustafa Bigham Mkuu wa Idara ya Mikoa ya Ustawi wa Utamaduni wa Qur'ani nchini Iran amesema maafisa husika katika mikoa yote 31 ya Iran wanajitahidi kufikia lengo hilo lililoainishwa katika Mpango wa Kitaifa ya Kuhifadhi Qur'ani.

Katika hotuba aliyotoa mwaka 2011, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyed Ali Khamenei alisema jamii ya Iran inapaswa kupanga mkakati wa kuhakikisha kuwa kuna Wairani milioni 10 waliohifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu.

Kwa msingi wa nasaha hiyo, taasisi husika za Qur'ani Tukufu nchini Iran zilianza kupanga mkakati ujulikanao kama 'Mpango wa Kitaifa wa Kuhifadhi Qur'ani' ambao unalenga kustawisha uwezo wa kuhifadhi Qur'ani Tukufu. Kwa mujibu wa ratiba ya mpango huo, inatazamiwa kuwa ifikapo mwaka 2025 kutakuwa na Wairani milioni 10 waliohifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu, Inshallah.

Kufuatia ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu mwaka 1979, Iran imekuwa katika mstari wa mbele wa kueneza harakati za Qur'ani kitaifa na kimataifa.

3464768

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: