IQNA

15:29 - May 27, 2018
News ID: 3471533
TEHRAN (IQNA)- Waislamu katika maeneo yote duniani wanaendelea na saumu ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ambapo baadhi ya maeneo muda wa saumu ni masaa 11 na baadhi ya maeneo karibu karibu masaa.

Kwa mujibu wa hesabu za kalenda ya Kiislamu ya Hijria Qamaria, tarehe ya kuanza Mwezi Mtukufu wa Ramadhani husonga mbele kwa karibu wiki mbili kila mwaka mkabala wa kalenda ya Miladia (Gregorian). Katika nchi zilizo katika ukanda wa ikweta zikiwemo nchi za Afrika Mashariki, masaa ya saumu ya Ramadhani huwa takribani masaa 12 miaka yote. Katika upande mwingine Waislamu wanaoishi katika nchi za ncha ya kaskazini katika eneo la Arctic, saumu ya mwezi wa Ramadhani hudumu kwa muda wa masaa zaidi ya 20 kwa siku. Kwa mfano nchini Iceland jua hutua saa sita usiku na kuchomoza baada ya masaa mawili katika kilele cha cha msimu wa joto.

Waislamu nchini Iceland wanatazamiwa kufunga hadi masaa 21 na dakika 51 mwaka huu mnamo Juni 14 katika siku inayotarajiwa kuwa ya mwisho katika mwezi mtukufu wa Ramadhani. Katika siku hiyo, jua linatazamiwa kutua saa tano na dakika 57 usiku.

Baadhi ya wanazuoni wanasema Waislamu wanaoishi katika nchi kama hizo ambazo mchana unapindukia masaa 20 wanaweza kufuata nchi zilizo karibu zenye masaa ya kawaida au mojawapo ya nchi za Kiislamu au pia wanaweza kufuata masaa ya nchi hiyo.

Karim Askari Mkurugenzi wa Taasisi ya Kiislamu ya Iceland anasema kukaa masaa 21 pasina kula ni changamoto kubwa lakini, aghalabu ya Waislamu katika mji wa Reykjavik, mji mkuu wa Iceland, kwa uwezo wake Allah, wanajitahidi kufunga saumu ya Ramadhani.

3465949

Name:
Email:
* Comment: