IQNA

18:12 - September 08, 2018
News ID: 3471663
TEHRAN (IQNA) - Wanaakiolojia huko Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE au Imarati) wamegundua msikiti unaokadiriwa kuwa uliojengwa miaka 1,000 iliyopita katika eneo unakojengwa Msikiti Mkuu wa Sheikh Khalifa mjini Al Ain karibu na mpaka wa nchi hiyo na Oman.

Magofu ya msikiti huo yametajwa kuwa ya zama za Ukhalifa wa Bani Abbas na yamepatikana karibu na falaj (njia za kumwagilia mashamba maji) na ulijumuisha kwa uchache majengo mtatu ya matofali.

Wanaakiolojia wa Idara ya Utamaduni na Utalii Imarati wanasema magofu ya msikiti huo yanaonyesha mihrabu ilivyokuwa na kwamba inakadiriwa kuwa waumini waliswali nje na ndani ya msikiti. Aidha wanaakiolojia wamepata mabaki ya vyungu ambavyo yamkini vilikuwa vikutumiwa kwa ajili ya maji ya udhuu au masuala mengine yanayohusiana na msikiti. Uchunguzi uliofanywa kwa kutumia mbinu ya radiocarbon umebaini kuwa msikiti huo ndio wa kale zaidi kuwahi kugunduliwa UAE hadi sasa.

3466725

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: