IQNA

Mashindano ya Qur'ani ya Majeshi ya Iraq

13:13 - November 28, 2018
Habari ID: 3471754
TEHRAN (IQNA)- Washindi wa Duru ya pili ya Mashindano ya Qur'ani ya Majeshi ya Iraq wametunukiwa zawadi katika sherehe iliyofanyika Jumanne.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA,  Saif Ali ametangazwa mshindi katika kategoria ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu.

Katika kuhifadhi Juzuu 10, Juzuu 5 na Juzuu 1 washindi walikuwa ni Hadi Taima, Yasir Ibrahim na Hakim Muhammad kwa taratibu.

Aidha katika kitengo cha qiraa, mshindi alikuwa ni Muhammad Zalif. Mchujo wa mashindano hayo ulifanyika Jumatano na Alhamisi wiki jana na wale waliofuzu waliingia katika fainali iliyofanyika Jumatatu na Jumanne wiki hii.

Washiriki wa mashindano hayo walikuwa ni kutoka vitengo mbali mbali vya majeshi ya Iraq na pia kutoka Jeshi la Kujitolea la Wananchi maarufu kama Hashd al Shaabi.

Jopo la majaji lilijumuisha maustadhi maarufu wa Qur'ani nchini Iraq wakiwemo Osama al-Karbalayi, Rafi al-Ameri and Abu Muhammad al-Jinabi.

3767671

captcha