Raef Al-Amiri, mkurugenzi wa Kituo cha Kitaifa cha Sayansi ya Qur'ani nchini Iraq na mjumbe wa Kamati Kuu ya Kuandaa Mashindano, ametangaza kuwa, Tuzo ya kwanza ya Qur'ani ya Kimataifa ya Iraq itafanyika mjini Baghdad kuanzia Jumamosi, Novemba 9, hadi Novemba 14, mwaka huu kwa ushirikiano na mashirika ya Wakfu ya Shia na Sunni.
Al-Amiri alibainisha kuwa mashindano haya yanawakilisha mpango wa kwanza wa ngazi ya serikali wa aina yake nchini Iraq na kwamba Waziri Mkuu Mohammed Shia’ Al-Sudani aliidhinisha tukio hilo mapema mwezi huu huko Baghdad.
Ameongeza kuwa, wahifadhi na maqari 31 wa Qur’ani Tukufu kutoka nchi za Kiarabu na Kiislamu watashiriki katika toleo hili la mashindano hayo.
Afisa huyo wa Iraq alisema kuwa lengo kuu la mashindano hayo ni kuangazia turathi za Qur'ani za Iraq na kuhimiza usomaji na kuhifadhi Qur'ani.
Alifafanua kuwa mashindano hayo yatafanyika kwa hatua mbili: hatua ya awali itashirikisha washiriki wote, wakati hatua ya pili itapunguza uwanja hadi washiriki watano bora.
Kwa mujibu wa mkurugenzi wa Kituo cha Kitaifa cha Sayansi ya Qur'ani, washindi watatunukiwa zawadi zenye thamani, na mashindano hayo yatafanyika chini ya kauli mbiu ya, “Kutoka Baghdad, Nembo ya Ustaarabu na Uislamu, hadi Gaza, Nembo ya Muqawama, na Lebanoni, Nembo ya Jihadi; Kupitia Qur’ani, Tunapata Ushindi na Uthabiti.”
3490607