IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Hafidh wa Iran aridhika na Masindano ya Qur’ani ya Iraq

21:28 - November 12, 2024
Habari ID: 3479740
IQNA - Ali Gholamazad ambaye anaiwakilisha Iran katika toleo la kwanza la Tuzo la Kimataifa la Qur'ani la Iraq amesema amefurahishwa na jinsi alivyofanya vyema katika shindano hilo.

Gholamazad anashindana katika kategoria ya kuhifadhi Qur’ani nzima. Alipanda jukwaani kujibu maswali ya majaji siku ya Jumatatu.
Walimuuliza maswali kutoka katika Sura Al-Ma’idah, Kahf, Jathiyah, na Ghashiyah kisha wakamtaka asome aya za Surah Al-Fajr. "Kwa bahati nzuri, nilifanya vyema," aliiambia IQNA baadaye.
Baadaye siku ya Jumatatu, ilikuwa zamu ya mwakilishi mwingine wa Iran, Mehdi Shayegh, kuonesha vipaji vyake vya Qur'ani.
Shayegh anaishindania Iran katika kitengo cha usomaji wa Qur'ani. Toleo la kwanza la Tuzo la Kimataifa la Qur'ani la Iraq lilianza Jumamosi mjini Baghdad na litaendelea hadi Novemba 14. Kwa mujibu wa waandaaji, wahifadhi na qari 31 kutoka nchi za Kiarabu na Kiislamu wanashiriki katika mashindano hayo. Lengo kuu la shindano hilo ni kuangazia urithi wa Qur'ani wa Iraq na kuhimiza usomaji na kuhifadhi Qur'ani, wanasema.

3490654

captcha