IQNA – Haram Takatifu ya Hadhrat Abbas (AS) katika mji wa Karbala nchini Iraq imetangaza tukio lake kubwa la Qur'ani, "Tuzo ya Kimataifa ya Al-Ameed ya Kuhifadhi Qur'ani," ambayo itafanyika kama mashindano ya televisheni yaliyo wazi kwa wasomaji kutoka nchi zote.

Mashindano hayo yanalenga kueneza mafundisho Qur'ani Tukufu na usomaji wake na kuonyesha vipaji na ujuzi wa washiriki.
Kulingana na tangazo lililotolewa kwa IQNA, wale wanaotaka kushiriki katika mashindano hayo lazima wafuate masharti haya ya jumla:

Ili kujiandikisha kwa shindano, washiriki wanapaswa kutuma video zao na taarifa zinazohitajika kwa akaunti ya shindano kwenye programu ya Telegram. Ikiwa wanakabiliwa na tatizo lolote kwa kutumia Telegram, wanaweza kutuma ujumbe kwa akaunti ya WhatsApp ya usaidizi kwa nambari: +9647760005311.
Kipindi cha kujiandikisha kitaanza Februari 3, 2024 na kumalizika Februari 16, 2024. Matokeo ya washiriki waliokubaliwa yatatangazwa Februari 17, 2024.