Mhifadhi wa Irani Ali Gholamazad, ambaye amesafiri hadi Baghdad kushiriki katika kategoria ya kuhifadhi Qur'ani nzima, aliiambia IQNA kwamba Sheikh Ahmed Ahmed Nuaina na Sheikh Ahmed Isa al-Misrawi kutoka Misri pamoja na maustadhi wa Qur'ani wa Iran Qassem Raziei na Mutaz Aghaei watahudumu kwenye jopo la majaji.
Amesema kuwepo kwa vigogo hao na wataalam wengine kutoka nchi mbalimbali katika jopo hilo kunaongeza thamani ya shindano hilo.
Mehdi Shayegh ni mwakilishi mwingine wa Iran, anayeshindana katika kategoria ya usomaji wa Qur'ani.
Toleo la kwanza la Tuzo la Kimataifa la Qur'ani la Iraq lilianza Jumamosi mjini Baghdad, kwa kushirikisha washindani, wasuluhishi, na maafisa wa Iraq litaendelea hadi Novemba 14.
Kwa mujibu wa waandaaji, wahifadhi na maqari 31 kutoka nchi za Kiarabu na Kiislamu wanashiriki katika toleo hili la mashindano hayo.
Lengo kuu la mashindano hayo ni kuangazia turathi za Qur'ani za Iraq na kuhimiza usomaji na kuhifadhi Qur'ani, wanasema.
3490633