IQNA

11:58 - May 09, 2019
News ID: 3471948
TEHRAN (IQNA) – Maonyesho ya 27 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Tehran yamepangwa kuanza Jumamosi 11 Mei katika mji mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Hayo yamedokezwa na Bw. Abdul Hadi Faqihzadeh, Naibu Waziri wa Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu Iran anayesimamia masuala ya Qur'ani Tukufu.

Amesema nara na kauli mbiu ya maonyesho hayo ya wiki mbili itakuwa ni "Qur'ani, Maana ya Maisha"

Bw. Faqihzadhe ambaye pia ni mkuu wa maoneysho hayo amesema matayarisho yalianza miezi mitatu iliyopita. Kati ya nchi ambazo zinashiriki katika Maonyesho ya 27 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Tehran ni pamoja na Uturuki, Iraq, Indonesia, Afghanistan, Russia na Pakistan ambayo ni mgeni wa heshima katika maonyesho ya mwaka huu.

Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani ya Tehran huandaliwa kila mwaka na Waizara ya Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu Iran na hufanyika katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Maonyesho hayo yanalenga kustawisha ufahamu na utamaduni wa Qur'ani Tukufu nchini Iran. Katika maonyesho hayo huwa kunaonyeshwa mafanikio yaliyofikiwa na Iran na nchi zingine duniani katika sekta ya Qur'ani Tukufu.

3809321

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: