IQNA

Rais Hassan Rouhani
18:46 - May 29, 2019
News ID: 3471976
TEHRAN (IQNA) - Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amebainisha kuwa Palestina na Quds ni nembo ya mapambano ya Waislamu wote na kuongeza kuwa Israel ni nembo ya wavamizi ulimwenguni wanaotaka kuwadhulumu Waislamu.

Akizungumza Jumatano katika kikao cha Baraza la Mawaziri mjini Tehran,  Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria namna mataifa yaliyodhulumika ya Yemen na Palestina yanavyopitia wakati mgumu katika kipindi hiki cha mwezi Mtukufu wa Ramadhani na kuongeza kuwa: "Wananchi madhlumu wa Yemen na Palestina hawatishwi wala kuogopeshwa na nchi vamizi na kwamba maadui hatimaye watalazimika kuondoka katika nchi hizo kutokana na kujitolea, kuwa imara na kusimama kidete wananchi hao wanaodhulumiwa".

Huku akiashiria namna Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekuwa ikiunga mkono taifa madhulumu la Palestina tokea ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu miaka 40 iliyopita, Rais Rouhani amesema Iran itaendelea na sera hiyo na kuongeza kuwa, mwaka huu wananchi wa Iran watajitokeza kwa wingi katika maandamano ya SIku ya Kimataifa ya Quds. Rais Rouhani amesema: " Kila mwaka katika Siku ya Quds, watu wetu hujitokeza kwa wingi wakiwa katika Saumu ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na katika hali zote za hewa, kwa lengo la kutangaza uungaji mkono wao kwa ukombizi wa Quds Tukufu na Taifa la Palestina. Wananchi wa Iran wanajitokeza kwa lengo la kuendeleza a njia aliyowaonyesha Imam Khomeini MA wakiwa wamebeba bendera ya Uislamu. "

Rais wa Iran amesema kuhamishwa ubalozi wa Marekani kutoka Tel Aviv hadi Quds, na 'Muamala wa Karnie, ni nukta ambazo zinayafanya  maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds mwaka huu kuwa na umuhimu mkubwa zaidi ya miaka iliyotangulia.

Inafaa kuashiria hapa kuwa, Ijumaa ya mwisho wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani ilipewa jina la Siku ya Kimataifa ya Quds na Imam Khomeini MA  Mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Ijumaa hii ya tarehe 31 Mei ni Ijumaa ya mwisho ya mwezi Mtukufu wa Ramadhani na inaadhimishwa kama Siku ya Kimataifa ya Quds. Mbali na miji yote ya Iran, maandamano ya kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Quds yanatazamiwa kufanyika pia katika maeneo mengine kote duniani kuanzia Ijumaa hadi Jumapili.  

3815563

Name:
Email:
* Comment: