IQNA

Siku ya Kimataifa ya Quds kuadhimishwa kwa njia ya intaneti Uingereza

13:05 - April 27, 2020
Habari ID: 3472710
TEHRAN (IQNA) – Siku ya Kimataifa ya Quds (Jerusalem) mwaka huu itaadhimishwa kwa njia ya intaneti kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa corona.

Kwa mujibu wa Tume ya Kiislamu ya Haki za Binadamu (IHRC) yenye makao yake London, kwa mara ya kwanza katika historia yake, Siku ya Quds nchini Uingereza itaadhimishwa kwa njia ya intaneti kutokana na janga la COVID-19.

IHRC imesema kufutwa maandamano ya siku ya Quds hakuna maana kuwa dunia imesahau kadhia ya Palestina na Siku ya Quds ambayo ni muhimu katika kalenda ya Kiislamu.

Waislamu na wasiokuwa Waislamu kote duniani Hudhimisha Siku ya Kimataifa ya Quds kwa lengo la kutangaza kufungamana kwao na malengo ya ukombozi wa ardhi za Palestina ambazo zinakaliwa kwa mabavu na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu hayati Imam Khomeini (Mwenyezi Mungu amrehemu) ndiye aliyeipa siku hiyo ya Ijumaa ya mwisho ya mwezi Ramadhani jina la Siku ya Kimataifa ya Quds kwa shabaha ya kuakisi dhulma ya kihistoria inayofanywa na madola ya Magharibi yanayodai kutetea haki za binadamu, dhidi ya watu wanaoendelewa kudhulumiwa na kukandamizwa wa Palestina na ardhi yao takatifu. Tokea ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran mwaka 1979, Siku ya Kimataifa ya Quds imekuwa ikiadhimishwa kupitia maandamano na makongamano  kote duniani.

Kwa wale wanaotaka kushiriki katika Siku ya Kimataifa ya Quds  wanaweza kushiriki katika mjumuiko wa intaneti Ijumaa Mei 22 kuanzia saa 10-12 kwa saa za Uingereza kwa njia ya YouTube na Facebook kupitia anuani ya #AlQudsDay2020.

3471271

captcha