IQNA

Rais Hassan Rouhani
16:40 - December 11, 2019
News ID: 3472271
TEHRAN (IQNA) Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amebainisha kuwa serikali ya Iran haijaghafilika hata kidogo katika kuvuruga njama za adui na vikwazo. Ameongeza kuwa, Iran itasambaratisha njama hizo za maadui kwa njia mbalimbali kukiwemo kuzidisha uzalishaji wa ndani na kufanya mazungumzo.

Akizungumza leo mjini Tehran katika kikao cha baraza lake la mawaziri, Rais Hassan Rouhani amesema kuwa njama za Marekani dhidi ya Iran, Iraq, Syria, Lebanon, Afghanistan, Pakistan, Yemen na nchi nyingine za eneo hili zitafeli kwa kushirikishwa wananchi.

Ameongeza kuwa hakuna shaka kuwa wananchi wa eneo hili wanaweza kusimama imara mbele ya njama za maadui; ambapo wananchi wa Iran pia siku zote wamekuwa mstari wa mbele katika uwanja huo. 

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran aidha ameashiria maendeleo ya nchi hii katika miaka ya baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu na kueleza kuwa: Maendeleo ya Iran katika sekta ya bioteknolojia imepelekea kujitosheleza kwa karibu dola bilioni moja na kuweza pia kuzuia uaguziaji kutoka nje ya nchi dawa na vifaa vinginevyo. Rais Rouhani amesema Iran iko mbioni kujitosheleza kikamilifu katika chanjo zote za mwanadamu ili iache kuagiza kutoka nje bidhaa hiyo muhimu.

3863388

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: