IQNA

15:47 - August 24, 2019
News ID: 3472097
TEHRAN (IQNA) – Wakuu wa eneo la Chechnya katika Shirikisho la Russia Ijumaa wametangaza kufungua msikito ambao wameutaja kuwa mkubwa Zaidi barani Ulaya.

Msikiti huo ambao umepewa jina la Msikiti wa Mtume Muhammad (SAW) umejengwa kwa usanifu majengo wenye mvuto na Waislamu 30,000 wanaweza kuswali ndani yake wakati moja. Wakuu Chechnya wameutaja msikiti huo kuwa 'mkubwa na maridadi zaidi' barani Ulaya.

Kiongozi wa eneo la Chechnya, Ramzan Kadyrov, ambaye ni muitifaki wa Rais Vladimir Putin wa Russia, amesema msikiti huo, ambao uko katika mji wa Shali ulio nje kidogo ya mji mkuu Grozny, una muundo adhimu, wa kipkee na maridadi.

Uwanja wa msikiti una mandhari ya kuvutia na umeandaliwa ili uweze kutumiwa na waumini wengine 70,000 na kwa msingi huo, kwa ujumla watu laki moja wanaweza kuswali hapo kwa wakati moja.

Kadyrov aliteuliwa na Rais Putin mwaka 2007 kuongoza eneo la Chechnya ambalo aghalabu ya wakaazi wake ni Waislamu na amekuwa mstari wa mbele kuhuisha Uislamu eneo hilo kwa kujenga misikiti na harakati nyinginezo.

Mwaka 2008, alizindua msikiti uliopewa jina la 'Ahmad Kadyrov' mjini Grozny ambapo Waislamu 10,000 wanaweza kuswali ndani yake.

Idadi ya Waislamu nchini Russia inakadiriwa kuwa watu milioni 25 kati ya watu milioni 145 nchini humo,.

Ahalabu ya Waislamu nchini Russia wanaishi katika mji mkuu Moscow na miji mingine mikubwa kama vile St. Petersburg and Yekaterinburg. Halikadhalika kuna idadi kubwa ya Waislamu maeneo kama vile Jamhuri ya Tatarstan, Jamhuri ya Bashkortostan, Jamhuri za Caucasus Kaskazini, Jamhuri za Caucasus au Kavkazia Kaskazini , Jamhuri ya Adygea, Jamhuri ya Chechnya, Jamhuri ya Dagestan, Jamhuri ya Ingushetia, Jamhuri ya Kabardino-Balkaria, Jamhuri ya Karachay-Cherkessia, Jamhuri ya Krasnodar Krai na Jamhuri ya Ossetia Kaskazini. Jamhuri zote hizo ziko katika Shirikisho la Russia lakini zina mamlaka ya ndani ya kujitawala.

Msikiti mkubwa zaidi Ulaya wafunguliwa Chechnya

Msikiti mkubwa zaidi Ulaya wafunguliwa Chechnya

Msikiti mkubwa zaidi Ulaya wafunguliwa Chechnya

Msikiti mkubwa zaidi Ulaya wafunguliwa Chechnya

3836866

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: