IQNA

Waislamu Russia

Mwanaume ahukumiwa jela nchini Russia kwa kuvunjia heshima Qur'ani

11:04 - February 29, 2024
Habari ID: 3478430
IQNA - Kijana mmoja amehukumiwa kifungo cha miaka 3.5 jela nchini Russia kwa kujunjia heshima nakala Qur'ani Tukufu.

Mahakama ya Jamhuri ya Chechnya nchini Russia ilimhukumu mtu huyo, Nikita Zhuravel, 20, kifungo cha miaka mitatu na nusu jela kwa kuchoma nakala ya Qur'ani Tukkufu, chombo huru cha habari cha Sotavision kiliripoti Jumanne.

Alikuwa amezuiliwa Mei 2023 kwa tuhuma za kuchoma hadharani kitabu kitakatifu cha Waislamu katika eneo la kusini la Volgograd.

Mamlaka za eneo hilo zilikubali ombi la watekelezaji sheria wa Chechnya kutaka Zhuravel isimamiwe katika eneo la Kaskazini mwa Caucasus.

Mahakama ya Wilaya ya Visaitovsky katika mji mkuu wa Chechnya wa Grozny ilimpata Zhuravel na hatia ya kuwaudhi waumini wa kidini na uhuni siku ya Jumanne.

Hakimu aliafikiana na waendesha mashtaka na kumpa Zhuravel kifungo cha miaka mitatu na nusu jela.

Kijana huyo alikuwa amekiri mashtaka ya kuwaudhi waumini wa kidini lakini akakana kwamba alitaka kuvuruga utulivu wa umma.

3487361

captcha