IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu

Wanajeshi wa Ukraine walaaniwa kwa heshima Qur’ani Tukufu

22:07 - March 18, 2023
Habari ID: 3476722
TEHRAN (IQNA) - Hatua ya hivi majuzi ya wanajeshi kadhaa wa Ukraine kuteketeza moto nakala ya Qur'ani Tukufu inaendelea kulaaniwa vikali , huku rais wa Jamhuri ya Chechnya katika Shirikisho la Russia akiapa kuwatafuta na kuwaadhibu wale waliohusika na kitendo hicho kichafu.

Sheikh Abdullah Jabiri, katibu mkuu wa Harakati ya Umma ya Lebanon alilaani kitendo hicho na kusema ni jaribio la kugeuza vita vya Ukraine kuwa vita vya kidini.

Amefananisha hatua hiyo na mashambulizi ya Wazayuni dhidi ya matukufu ya kidini na kuongeza kuwa, rais wa Ukraine anapaswa kutoa maelezo na kuwaomba radhi Waislamu.

Aliendelea kusema kuwa mashirika ya Kiislamu, Jumuiya ya Nchi za Kiarabu na mashirika ya haki za binadamu lazima yachukue msimamo wa wazi kuhusu jinai hiyo.

Muhammad al-Baghdad, mkurugenzi wa ofisi ya vyombo vya ya Baraza Kuu la Kiislamu la Algeria, pia alilaani uchomaji moto wa Qur'ani Tukufu, akieleza kuwa ni ukiukaji mkubwa wa maadili na vigezo vya kuheshimu matukufu ya imani na tamaduni tofauti.

Alisema matukio kama hayo na kimya cha Wamagharibi  ni ishara ya wazi ya mtazamo wa kinafiki wa Wamagharibi kwa tamaduni tofauti.

Ameongeza kuwa kukabiliana na jinai ya kuvunjia heshima Qur'ani Tukufu, iliyotokea siku chache tu baada ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kutoa wito wa kuheshimiwa matakatifu ya Waislamu, kunahitaji hatua za kivitendo na si kulaani tu.

Mwanazuoni wa Kiislamu wa Lebanon Sadiq al-Nablusi pia alikemea uchomaji wa Qur'an Tukufu unaofanywa na askari wa siasa kali za mrengo wa kulia wa Ukraine.

Akizungumza na  Televisheni ya RT, alisema tukio hilo linaendana na malengo ya itikadi itikadi kali nchini Ukraine inayotaka kuchochea na kuzidisha migongano ya kidini.

Alisema ina ujumbe kutoka kwa watu wenye itikadi kali wa Ukraine kwa wanajeshi Waislamu katika jeshi la Russia kwamba iwapo vita vitaendelea, watu wenye itikadi kali watalipiza kisasi kwa njia yoyote wanayoweza.

Quran Desecration by Ukrainian Soldiers Draws Widespread Condemnations

Wakati huo huo, kiongozi wa Chechnya Ramzan Kadyrov alishutumu kitendo hicho cha kufuru na kusema amejitolea kuwatafuta na kuwaadhibu wanajeshi wa Ukraine walioidharau Qur’ani Tukufu.

Alitaja hatua hiyo kuwa ni ishara ya ufashisti na ushetani na kusema atafanya kila awezalo kuwatafuta wahusika na kuwaadhibu.

Kadyrov pia alitoa zawadi kubwa kwa mtu yeyote atakayempata askari wa Kiukreni waliohusika na jinai hiyo..

Askari wenye itikadi kali katika jeshi la Ukraine hivi karibuni walisambaza video inayoonyesha wakiivunjia heshima nakala ya Qur’ani Tukufu.

Video ya TikTok iliyowekwa mtandaoni inawaonyesha wanajeshi wa Ukraine wakichana ukurasa kutoka kwa nakala ya Kurani na kuuweka kwenye moto, ambapo ulishika moto.

 4128783

captcha