IQNA

Sherehe za miaka 1,100 ya Uislamu Tatarstan

21:35 - December 16, 2021
Habari ID: 3474682
TEHRAN (IQNA)- Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Tatarstan katika Shirikisho la Russia, Marat Khusnullin, ameidhinisha mpango wa kusherehekea mwaka wa 1,100 tokea Uislamu uingie eneo hilo.

Katika sherehe hizo za mwaka 2022, kutakuwa na matukio 71 ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Msikiti wa Sobornaja ambao utajumuisha majengo kadhaa kama vile jingo la makumbusho , maktaba  na madrassah. Halikadhalika kutafanyika makongamano kadhaa ya “Russia na Ulimwengu wa Kiislamu” ambayo yatashirikisha Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC), Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) ambalo limepanga kufanya kikao cha 45 cha Kamati ya Turathi ya Dunia katika mji mkuu wa Tatarstan, Kazan.

Wakaazi wa Tatarstan ni wa kaumu ya Wabulgaria wa Volga na walisilimu zaidi ya miaka elfu moja iliyopita. Wakaazi wa Tatarstan daima wamekuwa wakiishi kwa amani na Wakristo wa jamii ya Othodoxi nchni Russia. Sherehe za maadhimisho ya kuwasili Uislamu Tatarstan ni ishara ya Waislamu na Wakristo kuishi kwa maelewano Russia kinyume na inavyoshuhudiwa Ulaya magharibi ambapo kunaenezwa chuki dhidi ya Uislamu.

3476953

captcha