IQNA

Jarida la Time
16:44 - August 25, 2019
News ID: 3472099
TEHRAN (IQNA) – Jarida la kimataifa la Time limetangaza orodha ya 'Maeneo 100 Bora ya Kutembelea Duniani 2019' na Bustani ya Qur'ani ya Dubai ni miongoni mwa maeneo hayo.

Orodha hiyo ina maeneo 100 duniani  ambayo yako katika vitengo vitatu tafauti vya 'kutembelea', 'Kulala' na 'Kula na Kunywa'.

Katika kitengo cha sehemu za kutembelea, Bustani ya Qur'ani ya Dubai katika Umoja wa Falme za Kiarabu imetajwa kuwa miongoni mwa maeneo bora zadi ya kutembelea.

Kwa mujibu wa jarida la Time, ubora wa sehemu hazingatiwei tu kwa mtazamo wa idadi ya wanaotembelea bali pia mvuto usio wa kawaida ambao haupatikani sehemu nyingine yeyote.

Aidha Jarida la Time limeandika kuwa, orodha hiyo ya 'Maeneo 100 Bora ya Kutembelea Duniani 2019' imetangazwa baada ya kupigiwa kura na wahariri, waandishi habari an wataalamu wa sekta ya utalii kote duniani ambao wamezingatia masuala kama vile, viwango, ubunifu, uvumbuzi na taathira.

Bustani ya Qur'ani Dubai ilizinduliwa Machi 2019 Umoja wa Falme za Kiarabu mjini Dubai katika eneo la Al Khawaneej ambapo wageni wanapa fursa ya kujifunza kuhusu miujiza ya Qur'ani Tukufu.

Lengo kuu la kuanzishwa bustani hiyo limetajwa kuwa ni kuwaleta pamoja watu wa tamaduni, dini na kaumi mbali mbali ili waweze kuona mafanikio ya Uislamu katika uga wa ekolojia ya mimea.

Bustani hiyo imejengwa katika eneo lenye ukubwa wa hekari 60 na mimea yote iliyoko hapo imetajwa katika Qur'ani Tukufu. Aidha bustani hiyo ina vivutio vingine kama vile maeneo ya watoto kucheza, Kona ya Umrah, jukwaa la wazi la tamthilia, na maeneo yanayoonyesha miujiza ya kisayansi ya Qur'ani Tukufu.

Manispaa ya Dubai imetangaza kuwa kwa sasa hakuna malipo yoyote kwa anayetaka kutembelea bustani hiyo lakini tiketi ya Dirhamu 5 inahitajika kuingia Nyumba ya Kioo na Pango la Miujiza katika bustani hiyo.

Bustani ya Qur'ani Dubai ni kati ya maeneo bora zaidi duniani

Bustani ya Qur'ani Dubai ni kati ya maeneo bora zaidi duniani +PICHA

Bustani ya Qur'ani Dubai ni kati ya maeneo bora zaidi duniani +PICHA

3469244

Tags: iqna ، bustani ، Qurani ، Dubai
Name:
Email:
* Comment:
* captcha: