IQNA

17:05 - September 16, 2019
News ID: 3472132
TEHRAN (IQNA) – Shirika moja la kutetea haki a binadamu limeitaka serikali ya China kuwaachilia huru watoto Waislamu wa jamii ya Uighur wanaoshikiliwa kinyume cha matakwa ya wazazi wao katika shule za bweni za serikali mkoani Xinjiang.

Katika taarifa Jumatatu, shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limesema: "Wakuu wa China wanashikilia idadi isiyojulikana ya watoto ambao wazazi wao nao wako katika vizuizi vya serikali. Watoto hao wanashikiliwa katika shule maalumu za bweni bila la idhini ya wazazi wao na wala wazazi hawana ruhusa ya kuona watoto wao."

Kwa mujibu wa taarifa karibu Waisalmu milioni moja wa jamii ya Uighur na jamii zingine za wanaozungumza Kituruki wanashikiliwa katika kambi maalumu za kuwapa mafunzo wa Kikomunisti kinyume cha matakwa yao  mkoani Xinjiang. Human Rights Watch inasema kuna Waislamu wengin ambao pia wanashikiliwa katika kambi zingine nchini humo.

Kamati ya Umoja wa Mataifa ya Kuangamiza Ubaguzi wa Rangi imesema imeandika ripoti kuhusu masaibu ambayo Waislamu wanakumbana nayo katika kambi hizo.

Uislamu ni kati ya dini tano ambazo zinatambuliwa rasmi na Chama cha Kikomunisti China ambapo kuna takribani Waislamu milioni 23 nchini humo.

Katika miaka ya hivi karibuni kumeongezeka sera za kuwakandamiza Waislamu katika nchi hiyo hasa katika jimbo la Xinjiang wenye Waislamu Zaidi ya milioni 10 kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi na misimamo mikali.

3469411

 

Name:
Email:
* Comment: