IQNA

Meja Jenerali Qassem Suleimani
9:53 - October 03, 2019
News ID: 3472157
TEHRAN (IQNA) - Meja Jenerali Qassem Suleimani Kamanda wa Kikosi cha Qods katika Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amefanya mahojiano kwa mara ya kwanza baada ya miaka 20 na kutoa ufafanuzi wa kina kuhusu vita vya siku 33 vya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Lebanon, Hizbullah, na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Vita hivyo vilijiri katika miezi ya Julai na Agosti mwaka 2006. Katika mahojiano hayo amesema iwapo vita hivyo vya siku 33 havingesimamishwa kupitia Umoja wa Mataifa, basi Jeshi la Israel lingeangamizwa.

Katika mahojiano aliyofanya na Ofisi ya Kulinda na Kusambaza Athari za Ayatullah Khamenei ambayo yalitangazwa Jumanne kupitia tovuti ya khamenei.ir, Meja Jenerali Suleimani amebaini kuwa baada ya Marekani kuvamia Iraq kijeshi na kuibua ghasia katika eneo, utawala wa Israel ulienga kutumia fursa hiyo kuangamiza Harakati ya Hizbullah. Ameongeza kuwa nchi za Kiarabu zilitangaza kwa siri kuwa tayari kushirikiana na utawala wa Kizayuni katika kuangamiza Hizbullah lakini njama hizo zilifeli.

Aidha amedokeza kuwa,baada ya wiki moja ya mashambulizi ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Lebanon alifika katika mkutano na Kiongozi Muadhamu na baada ya kuwasilisha ripoti yake, Kiongozi muadhamu alimfahamisha kuwa: "Mimi ninatasawari kuwa ushindi katika vita hivi utakuwa sawa na ule ushindi wa vita vya Khandaq."

3469561/

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: