IQNA

11:53 - November 28, 2019
News ID: 3472236
TEHRAN (IQNA) – Rais Reccep Tayyip Erdogan wa Uturuki ametoa wito kwa Umoja wa Mataifa na asasi zingine za kieneo kuitangaza Machi 25 kama Siku ya Kimataifa ya Mshikamano katika Kukabiliana na Chuki dhidi ya Uislamu.

Erdogan ameyasema hayo Jumatano mjini Istanbul katika Mkutano wa 35 wa Ngazi ya Mawaziri katika Kamati ya Kiuchumi na Kibiashara ya Jumuiya ya Ushirikiano wa Nchi za Kiislamu (COMCEC).

Rais wa Uturuki amesema wale ambao wanadai kutetea demokrasia na haki za binadamu wanajifanya hawasikii wala hawaoni lolote kuhusu ubaguzi na ukandamizaji wa Waislamu na wahajiri katika nchi zao.

Mnamo Machi 25, mwaka huu, Waislamu wasiopungua 50 waliuawa na wengine wengi kujeruhiwa wakati gaidi raia wa Australia alipomimina risasi katika misikiti miwili mjini Christchurch, New Zealand wakati wa Sala ya Ijumaa. Kufuatia tukio hilo, kumekuwa na mapendekezo kadhaa ya kuitangaza Machi 25 kuwa Siku ya Kimataifa ya Kukabiliana na Chuki Dhidi ya Binadamu.

Erdogan amesema utawala haramu wa Israel hauheshimu haki za Wapalestina na jambo hilo linahatarisha mustakabali wa nchi zote za eneo.

Ametahadahrisha kuwa, "wale ambao wanajaribu kuubadlisha mji wa Quds (Jerusalem), ambao ni mji mtakatifu kwa dini tatu (Uislamu, Ukristo na Uyahudi), kuwa kituo cha itikadi zao tu, wanafanya kosa kubwa."

Rais wa Uturuki amesisitiza kuwa nchi za Uturuki zinausiadia utawala wa Kizayuni wa Israel na hivyo kuchochea taharuki katika eneo. Aidha amesema Uturuki itaendele akuunga mkono haki za Palestina katika majukwaa yote.

3469982

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: