IQNA

Gaidi aliyeua Waislamu 51 msikitni New Zealand ahukumiwa kifungo cha maisha jela

15:32 - August 27, 2020
Habari ID: 3473108
TEHRAN (IQNA) –Mahakama nchini New Zealand imemhukumu kifungo cha maisha jela gaidi Brenton Tarrant baada ya kupatikana na hatia ya kuwaua Waislamu 51 wakati wa swala ya Ijumaa mwezi Machi mwaka jana katika mji wa Christchurch.

Hakimu aliyetoa hukumu hiyo Alhamisi amekiri kuwa hiyo si adhabu tosha kwa jinai ya iliyotendwa na gaidi huyo mwenye itikadi kuwa wazungu ni wanadamu bora zaidi watu wengine wote.

Jaji Cameron Mander wa Mahakama Kuu ya Christchurch amesema Tarrant hajaonyesha kujuta na hiyo hata akibaki jela umri wake wote, adhabu hiyo haiwezi kutosha kufidia jinai zake. Aidha amesema katika hukumu hiyo ya maisha gerezani, Tarrant hatakuwa na haki ya kuomba kupunguziwa adhabu.
"Jinai zako zilikuwa za kishetani sana kiasi kwamba hata ukifungwa hadi ufe gerezani bado hautaweza hautakuwa umeadhibiwa vya kutosha," alisema jaji wakati akitoa hukumu.  Adhabu ya kifo nchini New Zealand ilifutwa katika sheria iliyopitishwa mwaka 2007.

Tarrant, raia wa Australia mwenye umri wa miaka 29, alikiri kutekeleza mauaji ya watu 51 na kujaribu kuwaua wengine 40 na pia amekiri kutekelezx akitendo cha kigaidi katika hujuma ya ufatuaji risasi kiholela dhidi ya misikiti miwili mjini Christchurch.

Gaidi Tarrant pia ni mfuasi sugu wa  Rais Donald Trump wa Marekani ambaye ni mashuhuri kwa chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu.

Katika shambulizi la kigaidi la Machi 15 2019 katika misikiti ya Linwood na al-Noor mjini Christchurch, Waislamu 51 waliuawa shahidi na wengine karibu 50 kujeruhiwa.

Waendesha mashtaka wanasema Tarrant alikusanya risasi 7,000 kwa ajili ya kutekeleza hujuma hiyo na hivyo alipanga vizuri kitendo hicho cha kigaidi. Waziri Mkuu wa New Zealand Jacinda Adern ameunga mkono hukumu hiyo huku akisema anatumai hatalitaja tena jina la gaidi huyo huku akiongoza kuwa anastahiki kufungwa maisha.

3472399

captcha