IQNA

18:52 - January 11, 2020
News ID: 3472364
TEHRAN (IQNA) - Kundi la kigaidi la ISIS (Daesh) limedai kuhusika na hujuma dhidi ya msikiti nchini Pakistan ambapo watu wasiopungua 15 wamepoteza maisha.

Hujuma hiyo ilijiri katika msikiti huko Quetta, mji mkuu wa mkoa wa Baluchistan wakati wa sala ya Magharibi Ijumaa. Afisa wa ngazi za juu wa polisi ni miongoni mwa waliouawa katika hujuma hiyo ya kigaidi.
Kundi la ISIS limesema limetekeleza hujuma hiyo ambayo ilikuwa ikiwalenga wafuasi wa kundi la Taliban la Afghanistan. Msemaji wa Taliban Qari Mohammad Yusuf Ahmadi ametoa taarifa na kusema wafuasi wa kundi hilo walikuwa ndani ya msikiti wakati wa hujuma hiyo.

3470330

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: