IQNA

14:28 - January 13, 2020
News ID: 3472368
TEHRAN (IQNA) - Shirika la Ushirikkiano wa Nchi za Kiislamu (OIC) limelaani vikali hujuma ya bomu ambayo ililenga msikiti huko Quetta, Pakistan na kupelekea watu kadhaa kuuawa na kujeruhiwa.

Katika taarifa, Katibu Mkuu wa OIC Yousef al Othaimeen amebainisha masikitiko yake makubwa kufuatia hujuma hiyo ya kigaidi ambayo imelenga eneo la ibada la Waislamu na kuwaua watu wasio na hatua.

Al Othaimeen aidha ametuma salamu za rambirambi kwa serikali na watu wa Pakesitna pamoja na familia za waathirika.

Halikadhalika katibu mkuu wa OIC amekosoa vikali utumizi wa mabavu na kumwaga damu ya watu wasio na hatia na kusema hakuna kisingizio chochote kinachoweza kuhalalisha ugaidi.

Kundi la kigaidi la ISIS (Daesh) limetoa taarifa kuhusika na hujuma  hiyo dhidi ya msikiti nchini Pakistan ambapo watu wasiopungua 15 walipoteza maisha.

Hujuma hiyo ilijiri katika msikiti huko Quetta, mji mkuu wa mkoa wa Baluchistan wakati wa sala ya Magharibi Ijumaa. Afisa wa ngazi za juu wa polisi ni miongoni mwa waliouawa katika hujuma hiyo ya kigaidi.

3470345

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: