IQNA

11:07 - January 18, 2020
News ID: 3472381
TEHRAN (IQNA) – Nakala milioni 1.5 za Qur'ani Tukufu zimechapishwa katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kipindi cha miezi tisa iliyopita.

Hayo yamedokezwa na Taasisi ya Darul Qur'an Karim ambayo husimamia uchapishaji na usambazaji Qur'ani nchini Iran.

Ripoti hiyo imesema kuanzia Machi 21 hadi Disemba 21 2019, kulitolewa leseni 87 za kuchapisha Qur'ani Tukufu.

Taarifa hiyo imesema wataalamu wa Darul Qur'ani Karim wamehariri na kupitia Qur'ani zilizochapishwa ili kuhakikisha kuwa hazina makoss.

Kila mwaka maelefu ya nakala za Qur’ani huchapishwa nchini Iran na kusambazwa nchini na maeneo mengine duniani.

3872161

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: