IQNA

17:03 - February 12, 2020
News ID: 3472463
TEHRAN (IQNA) - Ismail Haniya Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) amemtumia ujumbe Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na akimpongeza yeye na taifa la Iran kufuatia maadhimisho ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Katika ujumbe wake huo Ismail Haniya amesifu na kushukuru misimamo mikuu ya Iran kuhusu suala la Palestina na uungaji mkono wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa wananchi na muqawama wa Palestina; na kumuomba Mwenyezi Mungu amjalie afya njema na ufanisi mkubwa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na kuiruzuku zaidi maendeleo na ustawi Jamhuri ya Kiislamu na taifa tukufu la Iran.   

Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yalifikia ushindi Februari 11 mwaka 1979 sawa na Bahman 22 mwaka 1357 Hijria shamsiya kwa uongozi wa Imam Khomeini (M.A). 

Wananchi katika Iran nzima ya Kiiislamu jana Jumanne walishiriki kwa wingi katika maadhimisho ya mwaka wa 41 wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu kama ilivyokuwa huko nyuma na kwa mara nyingine tena walitangaza utiifu wao kwa malengo ya Mapinduzi ya Kiislamu na kwa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu. 

3878250

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: