Kwa mujibu wa Taasisi ya EncyclopaediaIslamica ambayo inajishughuisha na uchapisha wa Kamusi Elezo ya Ulimwengu wa Kiislamu, jildi hii ya 27 ina maneneo 603,000. Kati ya maudhui ambazo zinapatikana katika jildi hii ni kuhusu Uislamu katika zama za sasa, historia ya Uislamu, jiografia, filosofia, sanaa na usanifu majengo.
Lugha asili ya jildi hii ni Kifarsi na ina kurasa 858. Taasisi ya EncyclopaediaIslamica ilianzishwa mjini Tehran mwaka 1983kwa lengo la kufanya uchunguzi na utafiti wa kitaalamu kuhusu Ulimwengu wa Kiislamu na Iran na hivi sasa kamusi elezo inayochapishwa na taasisi hiyo imetambuliwa kuwa ni yenye itibari zaidi katika masuala ya Ulimwengu wa Kiislamu.