IQNA

Utawala wa Kizayuni wa Israel wahujumu Ghaza na kutenda jinai

20:51 - February 24, 2020
Habari ID: 3472502
TEHRAN (IQNA) - Jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel jana Jumapili lilishambulia kwa mizinga eneo la Ukanda wa Ghaza na kumuua shahidi kijana wa Kipalestina, Mohammed Ali al-Naim aliyekuwa na umri wa miaka 27.

Baada ya mauaji hayo askari wa utawala wa Kizayuni wa Israel waliuvunjia heshima mwili wa kijana huyo kwa kutumia buldoza.
Jinai hiyo ya Wazayuni imekabiliwa na hasira kali za wanaharakati wa Kipalestina. Saraya al Quds, tawi la kijeshi la harakati ya Jihad Islami ya Palestina Jumapili ya jana ilivurumisha maroketi 20 dhidi ya vitongoji vya walowezi wa Kizayuni vilivyoko kandokando ya Ukanda wa Ghaza. Baada ya shambulizi hilo Israel ilishambulia eneo la Ukanda wa Gaza na kuua shahidi wapiganaji wawili wa Saraya al Quds.
Uchambuzi wa matukio hayo yote unaonesha kuwa, chanzo cha vita na mashambulizi haya mapya ya Israel ni tabia na sera za kutenda jinai za utawala huo habithi. Ukweli huu unaonekana wazi katika hatua ya askari wa utawala huo wa kuuvunjia heshima mwili na maiti ya kijana, Mohammed Ali al-Naim baada ya kumuua kinyama huko Ghaza. Mwenendo huu wa kutishia maisha ya Wapalestina na kuwavunjia heshima hata baada ya kuaua unaonesha waziwazi sera na siasa za utawala wa Kizayuni wa Israel.
Duru mpya ya vita na mashambulizi ya Wazayuni dhidi ya raia wa Palestina ni matunda ya awali ya mpango wa kibaguzi wa Muamala wa Karne uliopendekezwa na Rais Donald Trump wa Marekani na kuzinduliwa katika ikulu ya Whote House tarehe 28 mwezi uliopita wa Januari. Mpango huo unadhamini kikamilifu maslahi ya utawala haramu wa Israel na kukingia kifua jinai na uhalifu wa utawala huo dhidi ya Wapalestina.
Baada ya kuzinduliwa mpango huo, wachambuzi wa mambo walisema waziwazi kwamba hauwezi kutengeneza suluhu na mapatano na kwamba, kinyume chake, utazidisha uhasama na machafuko katika eneo la magharibi mwa Asia.

3470728

captcha