IQNA

10:02 - January 01, 2020
News ID: 3472322
TEHRAN (IQNA) – Jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel limewaua shahidi Wapalestina 149 katika mwaka uliopita wa 2019, aghalabu wakiwa katika Ukanda wa Ghaza.

Akizungumza Jumanne, Mohammed Sbeihat, Katibu Mkuu wa Mjumuiko wa Kiataifa wa Familia za Mashahidi wa Palestina amesema: "Wapalestina waliouawa na wanajeshi wa utawlaa wa Israel mwaka 2019 ni 149 ambapo 112 ni kutoka Ukanda wa Ghaa na 37 ni kutoka Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan."

Amesema aghalabu ya waliouawa ni Wapalestina walio na umri wa kati ya miaka 20-25 na kwamba wakuu wa utawala dhalimu wa Israel wamekataa kukabidhi miili 15 kwa familia zao.

"Watoto waliouawa ni 33, yaani takribani asilimia 32 ya idadi ya mashahidi, na hili ni ongezeko la asilimia tano ikilinganishwa na mwaka 2018," amesema Sbeihat.

Halikadhalika ameongeza kuwa watoto 12 Wapalestina waliuawa na wanajeshi wa utawala wa Israel.

"Mwezi uliokuwa na umwagikaji mkubwa zaidi wa damu ulikuwa Novemba, ambapo Wapalestina 44 waliuawa," amesema Sbeihat.

Katibu Mkuu wa Mjumuiko wa Kiataifa wa Familia za Mashahidi wa Palestina pia amesema kwa ujumla katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, Wapalestina 807 waliuawa shahidi na Israel hii ikiwa ni wastani wa watu 161 kwa mwaka.

Wapalestina wanapigania ukombozi wa ardhi zao ambazo zinaendelea kukaliwa kwa mabavu na utawala bandia wa Israel.

3868060

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: