IQNA

Hamas yaunga mkono uamuzi wa ICC dhidi ya Israel

10:08 - December 23, 2019
Habari ID: 3472297
TEHRAN (IQNA) -Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina (HAMAS imeunga mkono uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai unaonyesha kuwa hulka ya uvamizi na ukaliaji ardhi kwa mabavu ya Israel na kiwango cha dhulma ilizowafanyia wananchi madhulumu wa Palestina vimezidi kudhihirika mbele ya jamii ya kimataifa.

Katika taarifa siku ya Jumapili, msemaji wa Hamas Abdul Latif al Qanua amesema kuna haka ya kuunga mkono haki za Wapalestina kupitia kuwafikisha kizimbani watawala wa Israel kutokana na jinai zao zakivita dhidi ya Wapalestina.

Hatua zilizo dhidi ya ubinadamu na za ukiukaji sheria zinazochukuliwa na utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina zimekuwa zikilaaniwa mara kwa mara na taasisi za kutetea haki za binadamu na pia za kimataifa. Kutokana na kushtadi kwa hatua hizo za utendaji jinai, taasisi ya kimataifa yenye jukumu la kushughulikia jinai za kivita hivi sasa imepanga kuchunguza suala hilo.

Kuhusiana na suala hilo, Bi. Fatou Bensouda, Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC ametangaza kuwa amepanga kuchunguza jinai za kivita zilizofanywa na utawala wa Kizayuni katika ardhi za Palestina. Bensouda mnamo Ijumaa Disemba 20 alieleza kuhusu juhudi za mahakama hiyo za kuchunguza jinai za kivita zilizofanywa na utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Ghaza na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na kueleza kuwa: Jinai za kivita zimejiri katika eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na huko Quds mashariki. Hatua ya Mahakama ya ICC ya kuamua kuingilia suala hili ni matokeo ya ombi la miaka mitano sasa lililowasilishwa na Mamlaka ya Ndani ya Palestina. Raia wa Palestina pia wamekaribisha hatua hii ya Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC).

3470158

captcha