Kwa mujibu wa taarifa maelfu ya Wapalestina walihudhuria Sala ya Ijumaa katika misikiti mingine 200 mjini Quds na maeneo mengine ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
Kujitokeza kwa wingi waumini kushiriki katika sala ya jamaa jana alfajiri ni kama sehemu ya kampeni ya Alfajiri Adhimu.
Kamepni hiyo ilianza wiki chache zilizopita kwa lengo la kuuhami Msikiti wa Al Aqsa na maeneo mengine matakaitfu ya Wapalestina ambayo yanakabiliwa na hujuma na jma za Wazayuni..
Katika wiki za hivi karibuni wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wamekuwa wakiwashhambulia Wapalestina wanaoshiriki katika Sala ya Alfajiri na kuwakamata baadhi yao.