IQNA

22:35 - March 11, 2020
News ID: 3472554
TEHRAN (IQNA) – Kesi ya kwanza ya kirusi cha Corona imeripotiwa katika mji mtakatifu wa Makka nchini Saudi Arabia.

Hayo yamedokezwa na Muhammad Khalid al-Abd al-Ali, msemaji wa Wizara ya Afya Saudi Arabia ambaye amethibitisha kuwa mtu aliyeambukizwa ugonjwa wa COVID-19, maarufu kama kirusi cha Corona amepatikana mjini Makka.

Wizara ya Afya ya Saudia imesema kwa ujumla kuna watu 20 ambao wameambukizwa kirusi cha Corona katika ufalme huo.

Wiki iliyopita Saudi Arabia iliwapiga marufuku raia wa kigeni kutekeleza Ibada ya Umrah na Ziara katika Msiktii wa Mtume SAW.

Katika taarifa rasmi siku ya Jumatano, Wizara ya Mambo ya Nje ya Saudi Arabia imesema imeama: "Tumeamua kusitisha kwa muda Umrah kwa raia na wakaazi wa Saudia. Aidha Ziara katika Msikiti wa Mtume mjini Madina ni marufuku."

Taarifa hiyo ilisema lengo la uamuzi huo ni kuzuia kuenea kirusi cha Corona katika misikiti miwili mitakatifu ya Makka na Madina ambayo kwa kawaida hushuhudia msongamano mkubwa wa waumini. Kumekuwa na wasiwasi kuwa Saudi Arabia, ambayo hupokea karibu waumini milioni 7 kila mwaka kwa ajili ya Ibada ya Umrah, haijakuwa na uwazi kuhusu namna kirusi cha Corona kilivyoiathiri nchi hiyo.

3470883

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: