IQNA

10:32 - March 09, 2020
News ID: 3472546
TEHRAN (IQNA) – Wakuu wa Saudi Arabia Jumatatu Jumatatu wametangaza kusitisha shughuli zote za usomaji Qur'ani na mafundisho mengine misikitini kufuatia hofu ya kuenea ugonjwa wa COVID-19 maarufu kama Corona.

Aidha Wizara ya Elimu Saudia imetangaza kufungwa kwa muda shule na vyuo vikuu vyote nchini humo kuanzisha Jumatatu.

Halikadhalika wakuu wa Saudia wametangaza kupiga marufuku raia wa nchi hiyo na raia wa kigeni waishio nchini humo kutembelea Umoja wa Falme za Kiarabu, Kuwati, Bahrain, Lebanon, Syria, Misri, Iraq, Itali na Korea Kusini. Watu ambao wamesafiri katika nchi hiyo katika kipindi cha siku 14 zilizopita pia watapigwa marufuku kwa muda kuingia katika ufalme huo.

Hadi kufikia sasa watu 15 wameabukizwa kirusi cha Corona ambacho kimeenza hofu duniani kote.

Hadi hivi sasa virusi hivyo vimeshaenea katika nchi 103 duniani huku idadi ya watu wanaoambukizwa virusi hivyo ndani ya China ikizidi kupungua siku baada ya siku.  Takwimu za hivi karibuni kabisa zinaonyesha kuwa, zaidi ya watu laki moja na elfu sita wameambukizwa virusi vya Corona katika maeneo mbalimbali ya dunia ambapo 60,000 kati yao wamepona huku takribani 3,600 wakiaga dunia.

3470856

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: