IQNA

Haramein za Makka na Madina zafunguliwa baada ya kufungwa kutokana na Corona

19:29 - March 06, 2020
Habari ID: 3472537
TEHRAN (IQNA) – Serikali ya Saudia imefungua tena Msikiti Mtakatifu wa Makka (al-Masjid al-Ḥaram) na Msikiti Mtakatifu wa Mtume SAW (Al Masjid an Nabawi) baada ya kufunga kwa muda maeneo hayo mawili matakatifu (Haramein) kutokana na hofu ya kuenea kirusi cha Corona.

Televisheni ya Saudia imetangaza leo Ijumaa kuwa, maeneo hayo mawili matakatifu yamefunguliwa tena baada ya oparesheni maalumu ya usafi na kunyinyizia dawa ya kuangamiza kirusi cha Corona.

Alhamisi Saudi Arabia ilitangaza marufuku raia wake na wakazi wa nchi hiyo kutekeleza ibada ya Umrah katika mji Mtakatifu wa Makka au kuzuru Msikiti wa Mtume SAW katika mji wa Madina kwa hofu ya kuenea kirusi cha Corona ambacho kinaenea kwa kasi duniani.

Uamuzi huo unakuja baada ya ule wa siku chache zilizopita wa kuwapiga marufuku raia wa kigeni kutekeleza Ibada ya Umrah na Ziara katika Msiktii wa Mtume SAW.

Kwa sasa maarufu wa raia wa kigeni kutekeleza Ibada ya Umrah  au Ziyara katika Msikiti wa Mtume SAW mjini Madina ni marufuku. Hatahivyo raia wa Saudia na wakaazi rasmi wa nchi hiyo ambayo wanarejea kutoka safari za nje ya nchi watalazimika kusibiri siku 14 kabla ya kuingia katika maeneo hayo matakatifu.

Kuna watu watano walioambukizwa kirusi cha Corona nchini Saudia hadi sasa. Kumekuwa na wasiwasi kuwa Saudi Arabia, ambayo hupokea karibu waumini milioni 7 kila mwaka kwa ajili ya Ibada ya Umrah, haijakuwa na uwazi kuhusu namna kirusi cha Corona kilivyoiathiri nchi hiyo.

3883506

captcha