IQNA

15:41 - March 23, 2020
News ID: 3472595
TEHRAN (IQNA) – Sala za jamaa zimesitishwa kwa muda katika Msikiti wa Al- Aqsa katika mji wa Quds (Jerusalem) ili kuzuia kuenea kwa ugonjwa wa corona au COVID-19.

Kwa mujibu wa Wakfu wa Waislamu Quds, uamuzi huo umechukuliwa katika cha dharura siku ya Jumapili na  marufuku hiyo ya muda itaanza kutekeleza Jumatatu.

“Hatua hii ni ya muda lakini wafanyakazi na walinzi wataendelea na kazi zao kama kawaida.” Aidha taarifa hiyo imesema Adhana itaendelea katika Msikiti wa Al Aqsa nyakazi zoto kama kawaida.

Wakuu wa Msikiti wa Al Aqsa wamesema uamuzi huo ni kwa ajili ya kulinda afya na maisha ya Waumini.

Al – Aqsa ni Msikiti wa tatu kwa utakatifu katika Uislamu baada ya Misikiti Miwili Mitakatifu (Haramein) ya Makka na Madina ambayo nayo pia imefungwa kwa muda kutokana na hofu ya kuenea kirusi cha corona.

3470973/

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: