IQNA

10:30 - March 19, 2020
News ID: 3472582
TEHRAN (IQNA) – Algeria imesitisha sala za Ijumaa na kufunga misikiti yote nchini humo kwa kama ikiwa ni katika jitihada za kuzuia kuenea ugonjwa wa COVID-19 maarufu kama corona.

Kwa mujibu wa taarifa,  adhana itaendelea kama kawaida katika misikiti. Hatua hiyo ya Algeria inakuja siku moja baada ya muafaka baina yake na Tunisia kuhusu kufunga mipaka ya nchi kavu baina yao.

Rais Abdelmajid Teboune anasema ugonjwa wa COVID-19 ni janga ambalo linatishia usalama wa taifa na amewahakikishia wananchi kuwa serikali yake itafanya kila iwezalo kukabiliana na ugonjwa huo.

Hadi kufikia Jumatatu, Algeria ilikuwa na kesi 60 za corona na ilikuwa miongoni mwa nchi za kwanza barani Afrika kuripoti ugonjwa huo.

Ugonjwa wa Covid-19 hadi kufikia sasa umeshaua watu 8,700 kote duniani, huku idadi ya watu walioambukizwa virusi hivyo hatarishi ikiongezeka na kufikia watu 212,000.

3470954

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: