IQNA

9:58 - March 19, 2020
News ID: 3472581
TEHRAN (IQNA) – Idara ya Masuala ya Misikiti katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesema sala za jamaa zimesitishw kwa muda katika misikiti kote nchini ikiwa ni katika jitihada za kukabiliana na ugonjwa wa COVID-19 maarufu kama kirusi cha corona.

Katika taarifa iliyotolewa Jumatano 18 Machi, idara hiyo imesema misikiti pia haitakuwa na mijumuiko yoyote ile katika kipindi cha kusitishwa sala za jamaa. Hata hivyo amesema kutakuwa na adhana kama kawaida katika misikiti na itabakia wazi kwa wale ambao wanataka kuswali Furada (bila jamaa).

Aidha sala za Ijumaa pia zimesitishwa katika miji yote ya Iran.

Kwa mujibu wa taarifa ya jana Jumatano ya Wizara ya Afya ya Iran, hadi hivi sasa wagonjwa 5,710 wa kirusi cha corona au COVID-19 wameshapona humo nchini kati ya watu 17,361 walioambukizwa ugonjwa huo hadi hivi sasa nchini Iran. 1135 kati ya hao wamefariki dunia.

3886233

Tags: Iran ، misikiti ، corona
Name:
Email:
* Comment:
* captcha: