IQNA

15:12 - March 23, 2020
News ID: 3472594
TEHRAN (IQNA) – Saudi Arabia imeanza kutekeleza sheria ya kutotoka nje au curfew baada ya kuongezeka idadi ya watu walioambukizw augonjwa wa COVID-19 au corona nchini humo.

Kwa mujibu wa taarifa, Mfalme Salman ameamuru kuwa sheria ya kutotoka nje itekelezwe kila siku kuanzia saa moja usiku hadi saa 12 asubuhi kwa muda wa siku 21 ili kuzuia kuenea kwa ugonjwa wa COVID-19 nchini humo.

Hayo yanajiri siku chache baada ya wakuu wa Saudi Arabia kutangaza kufunga misikiti miwili mitakatifu ya Makka na Madina katika hatua ya aina yake kihistoria.

Msikiti Mtakatifu wa Makka (al-Masjid al-Ḥaram) na Msikiti Mtakatifu wa Mtume SAW (Al Masjid an Nabawi) imefungwa kwa muda usiojulikana kwa muda kutokana na hofu ya kuenea kirusi cha Corona.

Hadi sasa watu walioambukizwa COVID-19 nchini Saudi Arabia ni 511 ikiwa ni idadi kubwa zaidi miongozi mwa nchi za Kiarabu za Ghuba ya Uajemi.

3470974

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: