IQNA

19:36 - March 31, 2020
News ID: 3472621
TEHRAN (IQNA) – Serikali ya Somalia imeamuru madrassah za Qur'ani zifungwe ili kuzuia kuenea ugonjwa hatair wa COVID-19 au corona.

Katika taarifa siku ya Jumatatu, Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kidini ya Serikali ya Kifederali ya Somalia iimetangaza amri ya kufunga madrassah za Qur'ani na vyuo vyote vya idini kuanzia 31 Machi kwa muda wa wiki mbili ili kuzuia kuenea kirusi cha corona.

Taarifa hiyo imesema: "Lengo la uamuzi huu ni kuzuia kuenea kirusi cha corona na kulinda maisha ya watu katika jamii."

Hapo kabla pia Serikali ya Kifiderali ya Somalia ilikuwa imeamuru kufungwa shule na vyuo vikuu nchini humo ikiwa ni hatua za kuzuia kuenea corona. Hadi sasa watu watatu wamethibitishw akuambukizwa virusi vya corona nchini Somalia.

3888319/

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: