IQNA

22:24 - March 30, 2020
News ID: 3472618
TEHRAN (IQNA) - Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbulah ya Lebanon Sayyid Hassan Nasrallah anasema athari za ugonjwa wa COVID-19 (corona) zinaweza kupita zile za Vita vya Kwanza na vya Pili vya Dunia na kuibua mfumo mpya duniani.

Sayyid Nasrallah amesema katika hotuba iliyorushwa hewani Jumapili kwa njia ya televisheni kwamba ulimwengu unapitia kipindi kipya "kisicho na mfano katika karne mbili zilizopita" katika mapambano yake dhidi ya virusi vya corona.

Akiashiria kuwa janga la corona limeufanya ulimwengu uchanganyikiwe na kusababisha vifo, Sayyid Nasrallah amesema, kuna haja ya kujifunza somo na kupata ibra kutokana na hali liyopo hivi sasa kote ulimwenguni. Amesema madola makubwa kama Marekani yamechanganyikiwa na kushindwa la kufanya na kuzitaka nchi zote kushikamana na kuelekeza nguvu zao katika suala la kupambana na virusi hivyo ambavyo amesema ni adui wa pamoja wa wanadamu wote.

Vilevile ameashiria mashambulizi yanayoendelea kufanywa na Saudi Arabia na washirika wake dhidi ya taifa la Yemen wakati huu wa maambukizi ya corona na kusema, ulimwengu unapaswa kusitisha vita nchini Yemen.

Katibu Mkuu wa Hizbullah amesema: Wasaudia wanaendelea kushambulia watu waliodhulumiwa wa Yemen wakati huu ambapo dunia nzima inatafuta ufumbuzi wa jinsi ya kukabiliana na maambukizi ya ugonjwa wa COVID-19.

3470999/

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: