IQNA

Muungano wa kivita wa Saudia wahujumu maeneo 300 Yemen kwa muda wa siku saba

11:42 - April 08, 2020
Habari ID: 3472645
TEHRAN (IQNA) - Muungano vamizi wa Saudi Arabia na Imarati umeshambulia maeneo mbali mbali ya Yemen zaidi ya mara 300 katika kipindi cha siku saba zilizopita.

Hayo yamesema nwa Msemaji wa jeshi la Yemen Brigedia Jenerali Yahya Saree  ambaye amesema kuwa muungano vamizi wa Saudia na Imarati utakabiliwa na jibu la jeshi la Yemen iwapo utakariri mashambulizi hayo.

Brigedia Jenerali Yahya Saree amesema kuwa Saudi Arabia na washirika wake siku kadhaa zilizopita walishambulia mara 300 mikoa mbalimbali ya Yemen. Ameongeza kuwa hatua za kuibua mivutano na hatari za nchi hizo vamizi hazitapita hivi hivi bila maajibu na kusema ni jukumu la jeshi la Yemen kuwalinda raia na nchi yao.  

Vita vilivyoanzishwa na muungano vamizi chini ya uongozi wa Saudi Arabia huko Yemen, tarehe 26 mwezi Machi mwaka huu vimeingia katika mwaka wake wa sita. Mlingano wa vita hivyo ulibadilika katika mwaka wake wa tano ambapo jeshi na makundi ya kujitolea ya wananchi wa Yemen yalitoa kichapo kikubwa kwa Saudia na washirika wake na kuwasababishia hasara na maafa makubwa.

Inafaa kuashiria kuwa, Saudia ilianzisha mashambulizi dhidi ya Yemen mwishoni mwa mwezi Machi 2015 kwa lengo la kuiondoa madarakani Harakati ya Ansarullah na kumrejesha usukani Abdrabbuh Mansour Hadi, rais wa zamani wa nchi hiyo aliyejiuzulu na kukimbilia Riyadh.

Hata hivyo Saudi Arabia na washirika wake wameshindwa kufikia malengo yao hayo huku wakisababisha maafa makubwa ya kibinadamu ikiwa ni pamoja na kuwaua raia wasio na hatia. 

Idadi kubwa ya watoto na wanawake ni miongoni mwa waliopoteza maisha moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja kutokana na vita dhidi ya Yemen vinavyoongozwa na Saudia kwa himaya ya madola ya Magharibi hasa Marekani na utawala haramu wa Israel.

3471072

captcha