IQNA

Mamilioni ya Waarabu hatarini kuambukizwa corona kutokana na ukosefu wa maji ya kunawa mikono

18:34 - April 15, 2020
Habari ID: 3472667
TEHRAN (IQNA) – Watu milioni 74 wanaoishi katika nchi za Kiarabu zenye uhaba wa maji wanakabliwa na hatari kubwa ya kuambukizwa ugonjwa wa COVID-19 au corona kutokana na kuwa hawana maji na sabuni ya kunawa nyumbani.

Kwa mujibu wa ripoti ya Tume ya Kiuchumi na Kijamii ya Umoja wa Mataifa katika eneo la Asia Magharibi (ESCWA), miongoni mwa wanaokabiliwa na hatari ni watu milioni 31 nchini Sudan, zaidi ya milioni 14 katika nchi nchi inayokabiliwa na vita ya Yemen na wengine milioni 9.9 nchini Misri.

Taarifa hiyo imesema: “Katika hali ambayo duniani kote imeafikiwa kuwa kunawa mikono kwa kutumia maji safi na sabuni ni njia bora zaidi ya kukabiliana na ugonjwa wa COVID-19, kitendo hiki sahali kitakuwa ni kigumu katika eneo (la Asia Magharibi) ambalo watu milioni 74 hawana uwezo  wa kimsingi wa kunawa mikono.”

Taasisi hiyo imeongeza kuwa wakimbizi na watu wanaoishi maeneo yenye mizozo ni mzigo ziada katika jitihada hizo za kukabliana na corona.

Katibu Mtendaji wa ESCWA Rola Dashti amesema: “Ni jambo la dharura kuhakikisha kuwa watu wote wanapata majisafi na usafi wa mazingira bila gharama.”

ESCWA imesema wakimbizi  milioni 26 katika nchi za Kiarabu wako katika hatari zaidi ya kuambukizwa corona kwa sababu wanakusma hujuma za majisafi na usafi wa mazingira.

Taaisisi hiyo ya Umoja wa Mataifa imesema wati milioni 87 katika eneo la Asia Magharibi hawana uwezo wa kupata maji safi ya kunywa katika ndani ya nyumba zao na hivyo wanalazimika kuenda kuchota maji eneo la umma hali ambayo inahatarisha afya yao.

3471159

captcha