IQNA

Adhana misikitini yasikika kupitia vipaza sauti kwa mara ya kwanza katika historia ya Canada

0:46 - May 01, 2020
Habari ID: 3472720
TEHRAN (IQNA) – Waislamu nchini Canada wamepata fursa ya kusikia adhana misikitini kupitia vipaza sauti kwa mara ya kwanza kabisa katika historia ya nchi hiyo ya Amerika Kaskazini.

Kati ya hatua ambazo zimechukuliwa kuzuia kuenea ugonjwa wa corona au COVID-19 nchini Canada ni marufuku ya Waislamu kuswali katika misikiti na kwa msingi huo, baadhi ya misikiti imeruhusiwa kuwa na adhana kupitia vipaza sauti ili Waislamu waishio maeneo ya karibu waweze kusikia sauti ya adhana. Kwa kawaida nchini Canada adhana huwa ndani ya misikiti bila vipaza sauti.

Irsaad Bala, mwanachama wa bodi ya Msikiti wa Jamia Toronto anasema hatua hiyo inakaribiswa na Waislamu kwani kila Muislamu huwa na hamu ya kusikia adhana kupitia vipaza sauti.

Amesema ruhusa ya adhana imetolewa tu katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na  imechukuliwa kutokana na zuio la watu kutoka nje katika kipindi hiki cha janga la COVID-19  nachini humo.

Imam wa Msikiti wa Madina mjini Toronto Sheikh Sheeraz Mohammad amesema uwezekano wa kuwepo idhini ya kudumu ya kuadhini kupitia vipaza sauti itategemea maoni ya wasiokuwa Waislamu wanaoishi karibu na misikiti. Amesema wanajaribu kupada idhini ya kuendele akuadhini kupitia vipaza sauti lakini kwa masharti.

Uislamu ni dini inayoenea kwa kasi zaidi Canada ambapo Waislamu wameongezeka kwa asilimia 82 katika kipindi cha muongo mmoja uliopita. Hivi sasa Waislamu ni asilimia 3.2 ya watu wote milioni 35 nchini Canada.

Waislamu wamepewa nafasi katika serikali ya Canada na kwa mfano hivi sasa Waziri wa Familia, Watoto na Ustawi wa Jamii ni Ahmed Hussein ambaye ana asili ya Somalia.

3895565

captcha