IQNA

19:40 - May 16, 2020
News ID: 3472771
TEHRAN (IQNA) - Harakati ya Nujaba ya Iran imeilaani vikali televisheni Televisheni ya MBC ya Saudia ambayo imemvunjia heshima Shahidi Abu Mahdi al-Muhandis.

Nasr al-Shammari msemaji wa  Harakati ya Nujaba katika taarifa  ametoa wito kwa serikali ya Iraq na wanazuoni nchini humo kulaani televisheni hiyo.

Hivi karibuni televisheni hiyo ya utawala wa Aal Saud haikukomea hapo, bali katika hatua nyingine mpya imemtuhumu Shahidi Abu Mahdi al-Muhandis, aliyekuwa Naibu Mkuu wa Al-Hashdu-Sha'abi kuwa ni gaidi. Abu Mahdi al-Muhandis, aliuawa shahidi Januari 3, 2020 pamoja na Shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, aliyekuwa kamanda wa kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) pamoja na wanamuqawama wengine wanane, katika shambulio la kinyama lililofanywa na jeshi la kigaidi la Marekani karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad, Iraq.

Shahidi Al-Muhandis pamoja na Shahidi Soleimani walitoa mchango mkubwa sana katika vita vya kupambana na ugaidi katika eneo hili la Asia Magharibi hasa katika nchi za Iraq na Syria na kulinda umoja wa ardhi za nchi hizo. Hapana shaka yoyote kuwa, kama si hatua za kijihadi na za kujitoa mhanga zilizochukuliwa na makamanda na mashujaa kama Luteni Jenerali Shahidi Qassem Soleimani na Shahidi Abu Mahdi al-Muhandis, leo kundi la kigaidi la DAESH (ISIS) lingekuwa ndio tishio kubwa zaidi kwa nchi za Kiarabu; na hata miji mikuu ya nchi hizo pia ingeandamwa na kundi hilo la ukufurishaji.

Aidha hivi karibuni pi katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani, kanali hiyo ya televisheni ya MBC inayomilikiwa na Saudi Arabia ilianza kurusha hewani filamu za mfuatano ziitwazo "Ummu Harun" na "Makhraj 7". Lengo la filamu hizo ni kutaka kuutakasa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel ili uonekane ni utawala wenye utu na kuufanya ukubalike mbele ya fikra za waliowengi katika Ulimwengu wa Waarabu. Hata hivyo waliowengi katika Ulimwengu wa Kiarabu wamezikosoa vikali filamu hizo na kuifanya MBC ilazimike kusimamisha uoneshaji wa filamu ya Makhraj 7.

3899229

 

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: