IQNA

21:43 - May 19, 2020
News ID: 3472780
TEHRAN (IQNA) – Utawala wa jimbo la Java Mashariki nchini Indonesia umebatilisha idhini ya Sala ya Idul Fitr katika Msikiti wa Al Akbar mjini Surabaya baada ya wataalamu kuonya kuhusu matokeo mabaya ya mjumuiko wa watu wengi wakati wa kipindi hiki cha janga la COVID-19.

Katibu wa utawala katika jimbo la Java Mashariki Heru Tjhajono amesema wamutumia barua uongozi wa Msikiti wa Al Akbar, msikiti mkubwa zaidi mjini Surabaya, na kutangaza kubatilisha idhini ya awali ya Swala ya Idul Fitri msikitini hapo.
Katibu wa Msikiti wa Al Akbar Helmu M. Noor amesema wameweza kudiriki sababu za utawala kuchukua uamuzi huo. “ Ili kuzuia madhara ambayo hayakukusudiwa, Msikiti wa Al Akbar umeamua kuwa Swala ya Idul Fitr haitaswaliwa”.
Helmy amesema awali Msikiti wa Al Akbar ulikuwa umepanga kupunguza idadi ya watakaoruhusiwa kuswali Idul Fitra hadi waumini 4,000 ili kutekeleza sheria za watu kutokaribiana. Kwa kawaida msikiti huo una uwezo wa kubeba watu 40,000.
Mji wa Surabaya ndio ulioathiriwa vibaya na COVID-19 katika jimbo la Java Mashariki. Kwa ujumla hadi sasa watu 18,010 wameambukizwa COVID-19 nchini Indonesia na miongoni mwao 1,191 wameaga dunia.
3471470

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: