IQNA

Indonesia yasema itahakikisha chanjo yake ya COVID-19 ni Halali

19:23 - October 12, 2020
Habari ID: 3473253
TEHRAN (IQNA) – Serikali ya Indonesia imeanzisha jitihada za kuhakikisha chanjo COVID-19 itakayotumika nchini humo ni Halali, yaani haitakuwa na mada ambazo ni kinyume cha mafundisho ya Uislamu.

Waziri wa Uchumi Airlangga Hartarto, ambaye anasimamia  mpango wa kitaifa wa kukabiliana na COVID-19 na kuhuisha uchumi amesema serikali ya Indonesia inalenga kupata dozi milioni 320 za chanjo ya COVID-19.

Amesema serikali imeshauriana na Baraza la Maulamaa Indonesia ili kuhakikisha kuwa chanjo hiyo inapata cheti cha ‘Halal’.

Raia wengi wa Indonesia wamekuwa na wasi  wasi kuwa yamkini chanjo cha COVID-19 ikawa na mada ambazo ni haramu kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu. Maafisa wa serikali ya Indonesia wanatazamiwa kuitembelea China kuchunguza mchakato wa utegenejzai chanjo ya COVID-19 ili kuhakikisha kuwa haikiuki mafundisho ya Kiislamu.

Hadi sasa watu zaidi ya laki tatu 337,000 wameambukizwa COVID-19 Indonesia na miongoni mwao wengine karibu 12,000.

3472808

Kishikizo: indonesia covid 19
captcha