IQNA

Uturuki: Usitishwaji vita Libya si kwa maslahi ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa

22:37 - July 13, 2020
Habari ID: 3472960
TEHRAN (IQNA) -Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki amesema Serikali ya Muafaka wa Kitaifa Libya, inayotambuliwa na Umoja wa Mataifa, itaafiki mpatano ya usitishwaji vita iwapo tu jenerali muasi Khalifa Haftar ataondoa wapiganaji wake walioko maeneo ya kati na magharibi mwa nchi hiyo

Katika mahojiano na gazeti al Uingereza la Financial Times, Mevut Cavusoglu, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki amesema, Serikali ya Muafaka wa Kitaifa Libya (GNA) inayoongozwa na Waziri Mkuu Fayez al-Sarraj ina azma ya kuanzisha tena oparesheni za kijeshi dhidi ya wapiganajiw a Haftar iiwapo hawataondoka katika maeneo mawili ya kistratijia ambayo ni mji wa Bandarini wa Sirte na uwanja wa ndege za kijeshi katika mji wa Jufra.

Cavusoglu amesema Russia iliwasilisha pendekezo la usitishwaji vita katika mazungumzo yaliyofanyika Istanbul, Uturuki mwezi uliopita.

Amesema serikali ya Uturuki imewasiliana na Serikali ya Muafaka wa Kitaifa Libya ambayo imesema sharti la usitishwaji vita ni wanamgambo wa Haftar kuondoka Sirte na Jufra na kurejea katika maeneo waliyokuwa wanayasihikilia mwaka 2015.

Tokea Aprili 2019, wapiganaji wa Haftar walianzisha vita dhidi ya mji mkuu wa Libya, Tripoli na maeneo mengine ya kaskazini mashariki mwa Libya  na hadi sasa watu zaidi ya 1,000 wameuawa, ambao aghalabu ni raia, wakiwemo wanawake na watoto. Katika wiki za hivi karibuni jeshi la GNA limeweza kupata mafanikio makubwa katika vita dhidi ya wapiganaji wa Haftar ambao wametimuliwa kutoka mji mkuu, Tripoli na mji wa kistratijia wa Tarhuna.

Ni vyema kuashiria kuwa, Libya ina serikali mbili hasimu, moja ikiwa na makao yake mjini Tobruk, ambayo inapata himaya ya Jenerali Haftar, na nyingine ya Serikali ya Mapatano ya Kitaifa Libya inayoongozwa na Waziri Mkuu Fayez al-Sarraj inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa.

Wanamgambo hao wa Haftar wanategemea uungaji mkono wa Misri, Umoja wa Falme za Kiarabu , Saudi Arabia na baadhi ya nchi za Ulaya.

Libya ilitumbukia katika machafuko na vita vya ndani baada ya wanajeshi wa Marekani wakishirikiana na wale wa Shirika la Kijeshi la Nchi za Magharibi (NATO) kuishambulia nchi hiyo na kusaidia harakati za kumuondoa madarakani aliyekuwa kiongozi wa nchi Muammar Gaddafi hapo mwaka 2011.

3471991

Kishikizo: uturuki libya HAFTAR
captcha