IQNA

Kitabu kuhusu utamaduni wa Waislamu wa Ufilipino chazinduliwa

18:02 - July 22, 2020
Habari ID: 3472987
TEHRAN (IQNA) – Kitabu kuhusu Nafasi ya Waislamu katika Utamaduni wa Ufilipino kilichoandikwa na mwambata za zamani wa utamaduni wa Iran katika nchi hiyo ya kusini mwa Asia kimezinduliwa.

Kitabu hicho ambacho kimezunduliwa katika ofisi za Shirika la Habari la Qur'ani la Kimataifa mjini Tehran kimeandikwa na Mohammad Jaafari Malek, mwambata wa zamani wa utamaduni katika Ubalozi wa Iran nchini Ufilipino akishirikiana na Tandis Taqavi. Kitabu hicho chenye anuani ya "Waislamu wa Kusini mwa Ufilipino' kinaeleza kwa kina kuhusu historia, itikadi na utamaduni wa Waislamu wa nchi hiyo.

Jaafar Maleki anasema hujuma ya magaidi wa ISIS mwaka 2017 katika eneo la Mindanao, kusini mwa Ufilipino, ilikuwa cheche iliyompelekea afanya utafiti kuhusu hali ya Waislamu katika eneo hilo.

Amesema Waislamu wa Ufilipino hawana itikadi zinazoegemea upande wa magaidi wa ISIS. Ameongeza kuwa, tokea mkoloni Mhispania afike Ufilipino, Waislamu kusini mwa nchi hiyo wamekuwa katika harakati za kulinda utambulisho wao.

Ufilipino ni iliyo kwene Funguvisiwa la Malay katika eneo la kusini-mashariki mwa Asia. Ufilipino ina visiwa 7,641 vinavyohesabiwa katika makundi matatu yanayoitwa kufuatana na ujirani na visiwa vikubwa vya Luzon, Visaya, Mindanao.

Kwa mujibu wa takwimu, idadi ya Waislamu Ufilipino ni zaidi ya milioni 5.1, yaani asilimia 6 ya watu wote wa nchi hiyo. Zaidi ya nusu ya Waislamu wanaishi katika kisiwa cha kusini cha Mindanao.

3911997

captcha